Description
Oxford Revise and Assess ni msururu wa vitabu vya marudio ambavyo vimeangazia kikamilifu Mtaala wa Kiumilisi. Kila kitabu katika msururu huu kimefanyiwa utafiti wa kina na kuandikwa kwa utaalamu wa hali ya juu ili kukidhi mahitaji ya mwanafunzi katika udurusu wake. Vitabu hivi vinaangazia kwa kina mada zote kwenye mtaala ili kuwapa wanafunzi nguzo bora wanayoihitaji katika udurusu wao. Isitoshe, vitabu hivi vinamsaidia mwanafunzi kukuza umilisi wa kimsingi pamoja na kuwa atapata maarifa, ujuzi na maadili ambayo yatamwezesha kuwa na mtazamo chanya.
Katika Oxford Revise and Assess Kiswahili Gredi ya 7, utapata:
- Mpangilio wa sura unaoegemea stadi mbalimbali za lugha, yaani Kusikiliza na Kuzungunza, Kusoma na Kuandika, na vilevile Sarufi. Kila stadi imewekwa katika sura yake ili kurahisisha udurusu wa mwanafunzi.
- Shughuli 15 katika kila stadi. Shughuli hizi zinatokana na masuala makuu 15 katika mtaala. Katika kila shughuli, utapata mazoezi anuwa ya kushirikisha na kuchangamsha.
- Maelezo tangulizi kuhusu dhana mbalimbali ili kutoa ufafanuzi kwa dhana hizo.
- Muhtasari wa mambo muhimu ya kukumbuka kuhusu kipengele mahususi. Shughuli zenye kumshirikisha mwanafunzi katika matumizi ya vifaa vya kidijitali.
- Vifungu vya kusisimua, kuelimisha na kuzindua.
- Maelezo ya kina kuhusu uchambuzi wa kazi za kifasihi kwa kiwango hiki.
- Vielelezo mbalimbali na mwafaka vya insha katika sehemu ya Kuandika.
- Vielelezo vya tathmini tamati.
Reviews
There are no reviews yet.