Description
Tumalize anashangazwa na hatua ya baba yake kuwapa kitu fulani, watu fulani, kila siku asubuhi anapoenda shuleni. Kitendo cha baba yake kinamtia mshawasha wa kutaka kujua ni kitu gani hicho wanachopewa watu wale. Juhudi zake za kutafuta maelezo kutoka kwa baba yake kuhusu kitu hicho na sababu ya yeye kukitoa kwa watu wale zinagonga mwamba. Kwa sababu hiyo, anaapa kufanya juu chini ill apate kujua kitu hicho, na sababu inayofanya watu wale wapewe kitu hicho.
Je, Tumalize atapata kujua kitu hicho wanachopewa watu hao? Je, atafanya nini ili kubaini kitu hicho? Je, ni nini kitatokea atakapopata kugundua kitu chenyewe?
Twala Wapi Leo? ni kisa cha kusisimua cha kiupelelezi. Kisa hiki kinaangazia masuala ya malezi, elimu, ufisadi, ujasiriamali miongoni mwa masuala mengine katika jamii. Kisa hiki kimesheheni mbinu na mitindo mbalimbali ambayo itamfaidi mwanafunzi katika kujenga ubunifu wake na vilevile lugha yake.
Kuhusu mwandishi
Shullam Nzioka ni mwandishi, mfasiri, msawidi na ashiki wa lugha ya Kiswahili. Ameandika kazi mbalimbali za fasihi, zikiwamo novela, hadithi fupi na hadithi za watoto. Kitabu chake, Mbona Hivi? kilishinda tuzo ya Jomo Kenyatta Prize for Literature kitengo cha kijana mnamo mwaka wa 2021. Baadhi ya kazi zake zilizowahi kuchapishwa ni pamoja na Si Kitu na Shani ya Saa (hadithi fupi) iliyo katika kitabu Utashi wa Dola. Mbali na hayo, amewahi kufanya kazi katika shirika la International Bible Students Association.
Reviews
There are no reviews yet.