Uhuru wa Jelani

ISBN: 9789914442861Author: Wendo Nabea

KES 330.00

Je, unafikiri Jelani alihitaji uhuru wa aina gani? Je, ni nini kilichokuwa kimemsababishia ukosefu wa uhuru? Atafanya nini ili aweze kuupata uhuru huo? Je, atafanya nini iwapo ataupata uhuru huo?

Uhuru wa Jelani ni novela iliyosukwa kwa mtindo wa kipekee. Mwandishi ameyaweka bayana masuala ya kitamaduni ambayo yanaweza kutinga maendeleo ya mtoto msichana katika jamii ya leo. Novela hii imetumia mbinu anuai za lugha zinazoifanya hadithi yenyewe kuvutia na kumpa msomaji hamu ya kuendelea kusoma. Novela hii imeangazia masuala mtambuko mbalimbali na kusawiri maadili yanayopendekezwa katika Mtaala wa Daraja ya Awali ya Shule za Sekondari.

Kuhusu mwandishi

Wendo Nabea ni mtunzi wa tamthilia na bunilizi na kadhalika ni mhakiki wa fasihi. Ni mwelekezi, msahalishaji na mwamuzi katika Tamasha za Drama na Filamu na aidha Tamasha za Muziki za shule na vyuo nchini Kenya. Alipata shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Nairobi aliposoma Kiswahili na Fasihi ya Kiingereza na ambapo pia alisomea Uzamili. Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Vienna, Austria, kwa masomo ya Uzamifu. Hivi leo ni Profesa katika Chuo Kikuu cha Laikipia nchini Kenya anapofundisha Fasihi na Mawasiliano. Wendo Nabea ni mwandishi wa tamthilia Insha ya Siri iliyochapishwa na Shirika Ia Uchapishaji Ia Oxford.

Buy from Text Book Centre

Description

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Uhuru wa Jelani”

Your email address will not be published. Required fields are marked *