Kauli ya Leo: Diwani ya Mashairi

ISBN: 9789914442892Author: Oxford

KES 320.00

Kauli ya Leo ni diwani yenye mashairi arobaini, yakiwemo ya kiarudhi na huru. Mashairi katika diwani hii yameangazia masuala mbalimbali yanayoikumba jamii ya leo, kama vile majukumu ya kijinsia, utunzaji wa maliasili, uhuru wa wanyama, haki za watoto, teknolojia, magonjwa, lishe bora, usalama na uongozi bora.

Mashairi katika diwani hii yatamsaidia mwanafunzi kufikia matarajio yaliyowekwa na mtaala wa Gredi ya Tisa kuhusu vipengele vya ushairi, yaani wahusika, maudhui, dhamira, mbinu za lugha na muundo. Vilevile, yatawapa wanafunzi mtazamo mpana wa maisha pamoja na kuwapa changamoto ya kuwa wananchi waadilifu na wazalendo.

Watunzi wa mashairi haya, Bw. Ahmed Shikuku, Bw. Jackson Muraya, Bi. Ruth Omache na Bw. Evans Osoro, ni walimu wenye tajriba pana katika ufundishaji wa Kiswahili.

Diwani hii ina kiambatisho cha kidijitali ambacho kina maelezo ya kina kuhusu vipengele vya uchambuzi wa mashairi, uchambuzi wa baadhi ya mashairi pamoja na mazoezi ambayo yanaakisi matokeo maalumu katika mtaala wa Gredi ya 9 katika ushairi. Pia kina rekodi za mashairi hayo yakikaririwa au kughaniwa.
Maelezo hayo yako kwenye Msimbo huu wa QR.

Buy from Text Book Centre

Description

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Kauli ya Leo: Diwani ya Mashairi”

Your email address will not be published. Required fields are marked *