Description
‘Kiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha’ ni msururu wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa njia ya kipekee ili kutosheleza mahitaji ya mtaala mpya wa umilisi. Vitabu katika msururu huu vitamwezesha mwanafunzi kupata umilisi wa lugha katika stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika kama ilivyopendekezwa katika mtalaa mpya. Vitabu katika msururu vina mazoezi murua ambayo yatamchangamsha mwanafunzi na kumpa hamu ya kutaka kujifunza lugha. Mazoezi haya yanakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala ibuka.
‘Kiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha’, Mwongozo wa Mwalimu, Gredi ya 1 kina mifano halisi na ya kutosha kumwezesha mwalimu kuwasaidia wanafunzi kukuza umilisi unaokusudiwa. Katika mwongozo huu utapata:
- Utangulizi wa kina kuhusu mtalaa huu mpya wa umilisi.
- Muhtasari wa umilisi, maadili, masuala ibuka na shughuli nyinginezo zilizoratibiwa ufundishaji katika kila sura matokeo maalumu, maandalizi ya somo na shughuli za ufunzaji wa kila somo.
- Mapendekezo ya majibu ya maswali yote katika Kitabu cha Mwanafunzi.
- Mapendekeza ya shughuli za wanafunzi nje ya darasa.
- Maelekezo ya kina kuhusu jinsi ya kutathmini wanafunzi.
‘Kiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha’, Kitabu cha Mwanafunzi pamoja na Mwongozo wa Mwalimu vina shughuli, mazoezi na maelekezo tosha ambayo mwanafunzi na mwalimu watahitaji ili kufaulu katika mtaala huu mpya wa Umilisi.
Oxford, chaguo lako!
Reviews
There are no reviews yet.