Description
Ni vipi mtoto mdogo kama Sandra anafahamu maneno kama hayo? Tena maneno ambayo si ya Kiswahili, si ya Kiingereza, si ya lugha za kigeni au za kiasili. Yanatoka wapi? Ni nani waasisi wake? Mzee Jarida alijiuliza baada ya kumsikia mjukuu wake akizungumza. Maswali hayo yalipita akilini mwake haraka na kukaribisha fikra nyingi.
‘Mbona Hivi?’ ni riwaya ambayo imeandikwa kwa lugha yenye mvuto na upekee. Inaangazia masuala yanayoathiri vijana na kuibua mjadala – mjadala wa kujadiliwa leo, kesho na hata siku za usoni – kuhusu mustakabali wa lugha ya Kiswahili katika jamii.
Reviews
There are no reviews yet.