Description
‘Upeo wa Sarufi’ ni kitabu kilichoandikwa kwa utaalamu kikimlenga mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki kinaweza kutumiwa na mwanafunzi wa sekondari au wa chuo kama kitabu cha kiada au cha marejeleo.
Upekee wa kitabu hiki ni kwamba:
- Maelezo ya kina yametolewa kwa lugha sahili inayomwezesha mwanafunzi kuelewa vipengele vyote vya sarufi, hata bila ya usaidizi wa mwalimu.
- Matumizi ya lugha katika muktadha yanatiwa mkazo kuliko ukariri wa kanuni za sarufi.
- Mifano ya matumizi katika sentensi imetolewa kwa kila mada.
- Sehemu tata katika sarufi zimefafanuliwa.
- Kina mazoezi zaidi ya 200 na majibu yake.
- Kinatumia michoro na picha kurahisisha uelewa.
- Kinashughulikia silabasi nzima ya sarufi kwa sekondari, kama ilivyopendekezwa.
Kitabu hiki kimeandikwa na wataalamu wa lugha walio na ukwasi wa tajriba ya uandishi na ufunzaji wa sarufi ya Kiswahili.
Reviews
There are no reviews yet.