Description
‘Atamlilia nani?’ ni kitabu kinacholenga wanafunzi wa Darasa la Saba katika shule za msingi ili kuendeleza na kukuza uwezo wao wa kusoma. Miongoni mwa sifa za kipekee za kitabu hiki ni:
- Masimulizi rahisi kwa njia ya hadithi, mbinu rejeshi na uzungumzi nafsia.
- Kuingiza ucheshi katika maandishi kupitia masimulizi, dayolojia, misemo. methali, taharuki, tashibihi, takriri, kejeli, chuku, tanakali za sauti na picha za rangi zenye kusisimua.
- Kuwapitisha na kuwalea wanafunzi katika mazingira ya maisha ya nyumbani, malezi, afya, hatari ya kupenda sana mtoto, ujana na matatizo yake, utajiri na matatizo yoke, madawa ya kulevya na matatizo yake, umuhimu wa teknolojia, habari na mawasiliano, uwajibikaji, kazi, utu, uvumilivu, uadilifu, jinsia, haki za binadamu, haki za watoto, haki za wanyama, ukuaji wa kijiji kuwa mji na matatizo yake, kuishi kwa utangamano na amani.
Mradi wa Kusoma ni mfululizo wa vitabu vya ziada ambao unaambatana na kozi ua Kiswahili Sanifu.
Reviews
There are no reviews yet.