Description
‘Mashairi Bulbul’ ni kitabu kinacholenga wanafunzi wa Darasa la Saba katika shule za msingi ili kuendeleza na kukuza uwezo wao wa kusoma. Miongoni mwa sifa za kipekee za kitabu hiki ni:
- Mashairi yaliyobeba maudhui anuwai,
- Ubunifu wa mtunzi kutupambia mashairi kwa methali, mafumbo, masimulizi, tashihisi, takriri, tashbihi na taswira ili kutufunza na kupitisha ujumbe wake,
- Mitindo, bahari na aina mbalimbali za mashairi kama vile tathnia, tathlitha, tarbia, takhmisa, ukumi, ngonjera. utenzi, wimbo, ukaraguni, ukawafi, kikwamba na sakarani,
- Uangaziaji wa masuala ibuka kama vile dawa za kulevya, teknolojia, uadilifu, ushauri na nasaha, utatuzi wa matatizo, ubingwa wa lugha, vichekesho na burudani,
- Mradi wa Kusoma ni mfululizo wa vitabu vya ziada unaoambatana na kozi ya Kiswahili Sanifu.
Reviews
There are no reviews yet.