Description
Soma nasi, Kusoma na kuandika Kiswahili ni msururu wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa upekee ili kutosheleza mahitaji ya mtalaa mpya wa Umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika. Aidha, vina mazoezi murua ambayo yatampa mwanafunzi hamu ya kujifunza. Pia vinakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala ibuka.
Soma nasi, Kusoma na Kuandika Kiswahili, Kitabu cha Mwalimu, Gredi ya 2 kina mifano halisi na ya kutosha kumwezesha mwalimu kuwasaidia wanafunzi kukuza umilisi unaokusudiwa. Katika mwongozo huu utapata:
- Utangulizi wa kina kuhusu mtalaa huu mpya wa umilisi
- Muhtasari wa umilisi, maadili, masuala ibuka na shughuli nyinginezo zilizoratibiwa ufundishaji katika kila sura
- Matokeo maalumu, maandalizi ya somo na shughuli za ufunzaji wa kila somo
- Mapendekezo ya majibu ya maswali yote katika Kitabu cha Mwanafunzi
- Mapendekeza ya shughuli za wanafunzi nje ya darasa
- Maelekezo ya kina kuhusu jinsi ya kutathmini wanafunzi.
Soma nasi, Kusoma na Kuandika Kiswahili, Kitabu cha Mwanafunzi pamoja na Mwongozo wa Mwalimu vina shughuli, mazoezi na maelekezo tosha ambayo mwanafunzi na mwalimu watahitaji ili kufaulu katika mtaala huu mpya wa Umilisi.
Reviews
There are no reviews yet.