Description
Sarufi Dadisi (Gredi ya 4, 5 na 6) ni kitabu cha marudio ya sarufi kilichoandikwa kwa umakini mkubwa ili kuendana kikamilifu na mahitaji ya Mtaala wa Elimu ya Umilisi (CBE). Kitabu hiki kimefanyiwa ufatifi wa kina na kimeshughulikia mtaala mzima wa sarufi kwa shule za msingi.
Kimeandikwa kwa namna ya kipekee ya kukidhi mahitaji ya mwanafunzi katika udurusu wake.
Isitoshe, kitabu hiki kitamsaidia mwanafunzi kukuza umilisi wa kimsingi pamoja na kupata maarifa na ujuzi ambao utamwezesha kuwa na mtazamo chanya.
Katika Sarufi Dadisi (Gredi ya 4, 5 na 6) utapata:
- maelezo tangulizi kuhusu dhana mbalimbali ili kutoa ufafanuzi kwa dhana hizo.
- muhtasari wa mambo muhimu ya kukumbuka kuhusu vipengele mahususi.
- maelezo ya kina ambayo yametolewa kwa lugha sahili inayomwezesha mwanafunzi kuelewa vipengele vyote vya sarufi kwa urahisi.
- matumizi ya lugha katika muktadha yaliyotiliwa mkazo kuliko ukariri wa kanuni za sarufi.
- mifano ya kutosha ya matumizi katika sentensi kwa kila mada.
- shughuli za kutosha pamoja na majibu yake kwenye msimbo wa QR.
Kitabu hiki kimeandikwa na wataalamu wa lugha walio na ukwasi wa tajiriba ya uandishi na ufunzaji wa Kiswahili.




Reviews
There are no reviews yet.