Description
Musa, King Kong na wanafunzi wengine wa Bweni nambari 3 hawaamini kwamba kuna pepo. Lakini gimba hili la kutisha linalonyapanyapa kwenye uga wa shule yao ni kitu gani? Madoadoa ya ajabu ya ‘damu’ yametoka wapi? Na ni nani anayetoa kicheko cha kutisha nje ya mlango wa nyumba ya Bi Namukasa? Naibu wa mwalimu mkuu, Bw Karanja, anaamini kuwa ni wanafunzi wa Bweni nambari 3 wanaofanya mzaha. Kwa hivyo Musa na wenzake wanaamua kufanya juu chini kumnasa pepo huyu la sivyo atawafanya watimuliwe shule. ‘Musa na Pepo’ ni kitabu cha sita katika msururu wa Visa na Vituko vya Musa, vilivyoandikwa na Barbara Kimenye.
Reviews
There are no reviews yet.