Description
Wazo la kuanzisha shamba la shule linawafanya wanafunzi wa Mukibi’s Educational Institute for the Sons of African Gentlemen kuandaa mgomo baridi. Kwa madai yao wenyewe, wako shuleni ‘kusomea mitihani’ wala si kuwa mashokoa wa mwalimu mkuu, Mzee Mukibi. Hata hivyo, hakuna aliye tayari kumkabili mwalimu mkuu kwa kuhofia kuonekana muasi. Masaibu ya Musa na marafiki zake yanazidi kufuatia ‘kutoweka’ kwa nguruwe dume, na kuku sita kuibwa. Mwalimu mkuu naye ameapa kufanya juu chini kuwanasa wezi.
Reviews
There are no reviews yet.