Fani ya Isimujamii kwa shule za Sekondari

ISBN: 9780195734232Author: Ipara Isaac, Maina Godfrey

KES 525.00

‘Fani ya Isimujamii kwa Shule za Sekondari’ ni kitabu kitokanacho na juhudi za makusudi za kuziba pengo la ukosefu wa vitabu kwenye ufundishaji wa somo la Isimujamii katika shule za sekondari. Kitabu hiki kimeandikwa na wataalamu wenye tajriba pana katika taaluma ya lugha na ufundishaji wake. Ni zao la utafiti wa kina na tathmini ya mahitaji ya wanafunzi na jamii. Upekee wa kitabu hiki unatokana na jinsi kinavyozingatia mahitaji ya walengwa. Kitabu kimekusanya mada na vipengele vyote vya Isimujamii vilivyomo katika silabasi mpya na kuvizamia kwa uketo. Aidha, maudhui yameshughulikiwa kwa namna inayosisimua na kuchochea hamu ya wanafunzi na walimu. Maelezo nayo yametolewa kwa utoshelevu na kwa njia sahali inayobainisha kwa uwazi dhana na hoja ili kurahisisha usomaji na uelewa. Mifano kemkemi inayokita katika mazingira na miktadha halisi inayofahamika imetolewa ili kukipa kitabu nguvu za kipekee. Kila sehemu ina maswali yenye lengo la kuzindua fikira za walengwa, kuwapa mazoezi na kuwapiga msasa. ‘Fani ya Isimujamii kwa Shule za Sekondari’ kimeandikwa ili kukidhi kikamilifu mahitaji ya silabasi mpya ya Kiswahili na kuwapa wanaokitumia umilisi katika matumizi ya lugha kwenye nyanja mbalimbali. Kwa hakika kitabu hiki ni wenzo tosha kwa mwanafunzi anayejiandaa kuukabili ipasavyo, na kwa kujiamini, Mtihani wa Kiswahili wa Kitaifa wa Kidato cha Nne.

Buy from Nuria Kenya

Buy from Text Book Centre

Description

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Fani ya Isimujamii kwa shule za Sekondari”

Your email address will not be published. Required fields are marked *