Description
“Kivuli Kinaishi” ni tamthilia iliyoandikwa kwa kutumia dhana ya Giningi; makazi yaliyo ndani ya vichwa vya watu wa Unguja na Pemba na ambayo yanaogopwa sana na kuhusishwa na vitisho na hadithi kadhaa. Serikali ya Giningi yenye amri moja tu inaongozwa na Bi. Kirembwe akisaidiwa na wazee. Amali kuu ya Giningi imeonyeshwa kuwa ni ukatili na hivyo kanuni kubwa ni kujaribu kuwatoa watu kutoka dunia hii tuijuayo na kuwapeleka katika dunia ya siri, Giningi. Mwandishi amefaulu sana kutumia U-giningi katika kuchora picha fulani tata inayofanana na Giningi. Mhusika Mtolewa anadhihirisha mapambano ya kifikra yanayotokea kati ya wana-Giningi na Bi. Kirembwe na kuonyesha bayana mchezo huu unavyoambatana na ukweli wa maisha, na zaidi jinsi ulivyo mchezo wa wakati.
Reviews
There are no reviews yet.