Description
Inaichukua idara ya polisi zaidi ya miaka miwili bila kubaini chanzo wala sababu ya kuuawa kwa Mzee Majoro na mkewe, hali inayomtia mwanano Jackline wasiwasi mkubwa. Katika kutafuta haki, Jackline anamshirikisha mpelelezi Daniel Mwaseba kwenye harakati hizo, japo kwa siri. Uchunguzi wa Daniel unahusisha vifo hivyo na faili fulani ambalo limesababisha pia vifo na mateso kwa kila anayehusika kulisaka. Je, faili lenyewe lina nini? Je, Daniel atafanikisha msako huo uliowashinda hata wakuu wa polisi?
Msako Hatari ni kisa cha kijasusi kilichosukwa kwa upekee usio mfano. Mbali na kuwa kinaangazia maovu na udhalimu katika jamii, kinatoa mafunzo chungu nzima kuhusu haki na maadili.
Reviews
There are no reviews yet.