Description
Kwa nini Rehema alizaliwa tofauti na wazazi wake . . . ? Kwa nini alichaguliwa yeye kuwa ni ‘fumbo’?
la maumbile . . . ? Na kwa nini alifika duniani pale mama yake alipokuwa kapigwa na bumbuazi; baba yake yu katika hali iliyoelezewa kuwa huwafanya walioweka ahadi wazivunje, mashujaa wapoteze nguvu zao, matajiri wajione wahitaji, wenye macho wageuke pofu . . . ? Lakini hiyo ndiyo nyota ya Rehema.
llichomoza pale tete ya uzazi ilipotunga tumboni mwa mamaye. llimwongoza katika kiza cha majaaliwa– njia ya lazima kwa kila mja–akaifuata pasi na hiari. Vioja na vituko, siku nenda siku rudi, mpaka hatimaye amri isiyopingika ikasema, ho! Hapo ndiyo mwisho . . . .
Reviews
There are no reviews yet.