Description
Je, mbona Kolwa anataka kuozwa? Je, ni lazima akeketwe ndipo aozwe? Je, kwa nini Kolwa anafanya juu chini kuwazuia walezi wake kumwoza? Je, kwa nini Mzee Kausha anataka kumwoa Kolwa kuwa mkewe wa nne? Je, Kolwa ataweza kujitoa katika mipango ya walezi wake?
Haki ya Yahe ni tamthilia iliyoandikwa kwa weledi wa kipekee. Mwandishi ametumia lugha kwa namna inayoleta hamu kwa msomaji huku akiangazia mambo yanayotendeka katika jamii na mambo ambayo Watoto ambao hawana wazazi wanapitia. Tamthilia hii imeangazia masuala mtambuko mbalimbali na kusawiri maadili yanayopendekezwa katika Mtaala wa Daraja ya Awali ya Shule za Sekondari.




Reviews
There are no reviews yet.