Description
Dida anajenga urafiki wa dhati na Bobo, mwanafunzi mwenzake. Kupitia kwa Bobo, ambaye alimiliki simumaizi, Dida anapata fursa ya kujionea siyo tu mambo mbalimbali mitandaoni bali pia kuwasiliana na watu mbalimbali. Pale mtandaoni, marafiki hawa wanaajabia jinsi watu walivyoishi maisha mazuri na kuwafanya watake kuwa kama wao. Wanapatana na rafiki wa mtandaoni ambaye anawaahidi ajira yenye malipo mazuri ambayo yatabadilisha maisha yao.
Je, watachagua ajira ama masomo? Ni mwajiri gani huyu ambaye atawaajiri katika umri wao mdogo? Ni kazi gani hiyo ambayo watapewa?
Utando Hatari ni kisa kilichosimuliwa kwa ufundi wa aina yake. Kinamteka msomaji kutoka mwanzo na kumsafirisha pamoja na wahusika mpaka mwisho wa safari yao. Aidha, kinatahadharisha dhidi ya shinikizo la rika kwa kuonyesha jinsi mashinikizo kama hayo yanavyoweza kumtia mtu kwenye mitego ya wajanja.




Reviews
There are no reviews yet.