Fani ya Fasihi Simulizi kwa Gredi ya 7, 8 na 9

ISBN: 9789914445510Author: Assumpta Matei

KES 916.00

Fani ya Fasihi Simulizi kwa Gredi ya 7, 8 na 9 kimeandikwa kwa utaalamu mkubwa ili kufanikisha kikamilifu ufundishaji na ujifunzaji wa fasihi simulizi katika kiwango hiki. Kitabu hiki kimeshughulikia kwa kina na kwa njia ya wazi na nyepesi tanzu na vipera vya fasihi simulizi katika mtaala wa Gredi ya saba hadi Gredi ya Tisa.

Katika kitabu hiki, utapata:

  • Ufafanuzi wa kina wa dhana ya fasihi kwa jumla na hususan fasihi simulizi.
  • Uchanganuzi wa kina wa tanzu na vipera lengwa vya fasihi simulizi na mifano maridhawa.
  • Tunga za kuchanga, kusisimua na vilevile kurahisisha ujifunzaji.
  • Shughuli zenye kushirikisha kikamilifu katika ujifunzaji.
  • Tathmini endelevu za kumwezesha mwanafunzi kujitathmini na kutathminiwa na wenzake au na mwalimu.
  • Tathmini ya mwisho wa sura ili kumpa mwanafunzi picha ya jumla kuhusu kiwango chake cha ufahamu wa utanzu na kipera husika.
  • Mazoezi murua yanayochochea ujifunzaji huku yakipima ngazi zote za maarifa au utambuzi.
  • Tathmini tamati yenye mazoezi na maswali anuwai yatayomwezesha mwanafunzi kupima umilisi wake na kumtayarisha kwa Tathmini ya Mwisho wa Gredi ya Tisa- KJSEA.
  • Majibu kwa Tathmini tamati ili kumwelekeza mwanafunzi kubuni mikakati ya kujiboresha.

Dkt. Assumpta K. Matei ni msomi mwenye tajriba pana katika masuala ya elimu, utafiti, ufundishaji na tathmini. Ana uzoefu mkubwa katika ufundishaji wa Isimu, Lugha na Fasihi ya Kiswahili nchini Kenya. Baadhi ya vitabu alivyoandika ni pamoja na: Fani ya Fasihi Simulizi kwa Shule za Upili na Zawadi ya Thamani (novela). Vilevile, amashirikiana na wengine kuandika vitabu kama vile: Jipe Moyo (Diwani ya Mashairi), Kamusi ya Watoto na Upeo wa Ufahamu na Ufupisho.

Buy from Text Book Centre

Description

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Fani ya Fasihi Simulizi kwa Gredi ya 7, 8 na 9”

Your email address will not be published. Required fields are marked *