Description
‘Soma nasi, Kusoma na kuandika Kiswahili’ ni msururu wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa upekee ili kutosheleza mahitaji ya mtalaa mpya wa Umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika. Aidha, vina mazoezi murua ambayo yatampa mwanafunzi hamu ya kujifunza. Pia vinakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala ibuka.
Katika ‘Soma nasi, Kusoma na kuandika Kiswahili’, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi 1, utapata:
- Mada zilizopangwa kwa kuzingatia mtalaa.
- Mifano halisi ya miktadha ambapo lugha hutumika.
- Mazoezi nje ya darasa ili kuendeleza ujifunzaji.
- Mazoezi yanayomhusisha mwanafunzi moja kwa moja.
- Jinsi ya kuwashirikisha wazazi na walezi ili kuimarisha uwajibikaji.
- Sehemu ya ‘Tujifurahishe’ inayolenga kuwasisimua wanafunzi wanapotumia lugha.
‘Soma nasi, Kusoma na kuandika Kiswahili’, Kitabu cha Mwanafunzi kina Mwongozo wa Mwalimu ambao pia una mazoezi na maelekezo tosha ambayo mwalimu atahitaji ili kumwongoza mwanafunzi aweze kufaulu katika mtalaa huu mpya wa Umilisi.
Reviews
There are no reviews yet.