Description
‘Vitendawili kwa Mashairi’ 5b ni kitabu kinachonuiwa kuendeleza msingi wa kusoma na kukuza uwezo wa kusoma wa wanafunzi wa Darasa la Tano katika shule za msingi.
Miongoni mwa sifa za kipekee za kitabu hiki ni:
- Mashairi mepesi ya tarbiya ya beti moja moja.
- Umahiri wa mtunzi wa kutoa majibu ndani ya beti.
- Mtindo maalumu wa kutega na kutegua vitendawili kwa njia ya mashairi.
- Kuwapitisha na kuwalea wanafunzi katika mazingira ya chemsha bongo au vitendawili ili kukuza na kupanua fikra zao.
- Kurahisisha ufahamu ili kupata jibu la kila kitendawili kwa kuunganisha herufi au silabi fulani zilizomo ndani ya kila ubeti pamoja na kupitia picha zenye kusisimua na zenye rangi za kupendeza.
Mradi wa kusoma ni mfululizo wa vitabu vya ziada unaoambatana na kozi ya Kiswahili Sanifu.
Reviews
There are no reviews yet.