Description
Tito alijua kwamba hii ndio nafasi ya pekee aliyokuwa nayo ya kujinasua. Alijua kuwa ujasiri wake tu ndio ungemwokoa. Tito alikabiliwa na hatari kubwa. Hatari hii ilitishia kumpoteza kwao milele. Hatari hii ingemtenganisha na wazaziwe na nduguye, Jesi, daima. Tito aliogopa haya. Aliogopa sana. Ndiyo maana aliamua kujijasiri. Alijua kuwa ujasiri huu huenda ungemletea adhabu kali, lakini hakuwa na budi ila kujitwika ujasiri huu. Ilimbidi afanye lolote, ajikakamue, mradi tu ajiokoe! ‘Ujasiri wa Tito’ ni mojawapo ya hadithi katika mradi wa kusoma. Huu ni mradi wa vitabu vya ziada unaoambatana na kozi ya Kiswahili Sanifu.
Reviews
There are no reviews yet.