Description
Visa na Vituko vya Musa ni tafsiri ya Moses Series vilivyoandikwa na Barbara Kimenye, na ambavyo vinaangazia hali ya maisha ya wanafunzi shuleni mwao. Mbali na kuwa vinaburudisha na kuchekesha kwa visa mbalimbali vinavyomkumba Musa, yapo mafunzo mengi anayopata msomaji. Tafsiri hizi zinadumisha mvuto na mnato wa kazi asilia, na zitakupa shauku ya kusoma hadithi yote ili kujua hatima ya kisa chenyewe. Si jambo geni kwa Musa kuwa mashakani. Safari hii, yeye na marafiki zake katika Mukibi’s Educational Institute for the Sons of African Gentlemen wanafanya mgomo wa kimzaha kuhusu chakula wanachopewa shuleni. Mwanzoni, wanauona mzaha huo kuwa murua. Hata hivyo, Mwalimu mkuu, Bw Mukibi, hafurahishwi – yeye si mtu wa kuficha hisia zake.
Reviews
There are no reviews yet.