Description
Kwa nini Rehema alizaliwa tofauti na wazazi wake . . . ? Kwa nini alichaguliwa yeye kuwa ni ‘fumbo’ la maumbile . . . ? Na kwa nini alifika duniani pale mama yake alipokuwa kapigwa na bumbuazi; baba yake yu katika hali iliyoelezewa kuwa huwafanya walioweka ahadi wazivunje, mashujaa wapoteze nguvu zao, matajiri wajione wahitaji, wenye macho wageuke pofu . . . ? Lakini hiyo ndiyo nyota ya Rehema.
llichomoza pale tete ya uzazi ilipotunga tumboni mwa mamaye. llimwongoza katika kiza cha majaaliwa- njia ya lazima kwa kila mja-akaifuata pasi na hiari. Vioja na vituko, siku nenda siku rudi, mpaka hatimaye amri isiyopingika ikasema, ho! Hapo ndiyo mwisho . . .
Mohamed Suleiman Mohamed amezaliwa tarehe 5 Oktoba 1943, kijijini Koani katika sehemu ya kati ya kisiwa cha Unguja. Hamu yake ya kuandika ilimwanzia shuleni, ikamea alipotolewa uwanjani na BBC katika mwaka 1968. Hadithi yake kubwa ya mwanzo, Kiu, ilishinda mashindano ya Afrika Mashariki, na kupewa zawadi ya mwanzo na Mheshimiwa Rais Nyerere katika mwaka 1970. Katika mwaka 1973 amepewa tunza iliyofuatia ‘Kenyatta Prize for Literature’, Kenya, na pia amepata ushindi katika mashindano ya waandishi wa Tanzania. Vile vile ameandika hadithi fupifupi zilizokusanywa katika kitabu kiitwacho Kicheko.
Reviews
There are no reviews yet.