Description
‘Waja leo’ ni mkusanyiko wa mashairi ya aina yake yanayomulikia kurunzi vipengele anuwai vya waja (binadamu) wa leo. Watunzi wa mashairi katika diwani hii wana tajiriba na falsafa tofautitofauti zinazodhihirishwa na mitindo na maudhui yao mbalimbali. Mashairi yenyewe yameandikwa kwa lugha rahisi kusomeka na kueleweka, yaliyo na mvuto wa ajabu na ambayo yatawafaa wapenzi na wasomi wa mashairi ndani na nje ya mipaka ya asasi za elimu.
Katika diwani hii, mna utangulizi kwa msomaji wenye maelezo mwafaka kuhusu mbinu ya kuyasoma na kuyachambua mashairi kwa faida ya wasomaji katika shule za upili. Aidha, kuna maswali ya mazoezi kwenye kurasa za mwisho.
Reviews
There are no reviews yet.