Description
Mazungumzo yao yalikuwa mafupi. Alihitajika nyumbani haraka. Kulikuwa na dharura. Je, nini kilichokuwa kimetokea cha kuibua dharura hii? Ni kipi cha dharura ambacho hakingeweza kupitishwa kwa simu? Si simu zenyewe zinafaa kupitisha jumbe za dharura?
‘Wema Waliobaki’ ni riwaya inayoakisi sura mbalimbali za maovu yanayotekelezwa na watu wenye tamaa ya kuvuna wasichokipanda katika jamii ya leo. Ni hadithi inayowasawiri wanaja mii kama nduli wala watu; mamba wanaosubiri kwenye kingo za mito kuwavamia watekamaji wasiokuwa na habari. Hata hivyo, katika jamii iliyogubikwa na giza la ukosefu wa maadili hapakosi mwanga; mwanga unaotokana na wema waliobaki, hata kama ni wachache.
Reviews
There are no reviews yet.