Description
Katika juhudi zao za kutafuta mafuta, Tajeer na marafiki zake, wawekezaji wa kutoka ng’ambo, wameligeuza Ziwa Riziki kuwa tope jeusi na hivyo kuyaharibu maisha ya watu wengi waliolitegemea. Tajeer amefyeka misitu na kukausha vijito vinavyoihuisha jamii. Lengo lake ni kuanzisha mradi wa mamilioni ya pesa. Hata hivyo, Kibichi na familia yake hawako tayari kufurushwa kutoka kwenye ardhi ya wahenga wao. Kijani, binti shujaa wa jamaa hii, anajitolea kupambana na wavamizi hawa. Je, Tajeer na matajiri wenzake watafaulu?
Austin Bukenya ni mmoja wa wandishi mashuhuri wa kazi za fasihi katika Afrika Mashariki. Kando na kuwa mwandishi wa tamthilia, riwaya, ushairi na kuwa mhakiki mtajika, amefunza lugha, fasihi na maigizo katika vyuo vikuu nchini Tanzania, Uskoti, Ujerumani, Kenya na Uganda. Kitula G. King’ei, mfasiri wa tamthilia hii, ni profesa wa taaluma ya Kiswahili katika Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Mbali na kuchapisha makala na vitabu vingi vya kiada na vya fasihi, Profesa Kitula ametafsiri na kuhakiki kazi nyingi. Miongoni mwa kazi zake nyingi za kubuni ni pamoja na Mwili Wangu, Posa za Bikisiwa, Mgeni Mbaya na Ndoto ya Siti.
Reviews
There are no reviews yet.