Oxford Kamusi Maridhawa ya Methali

ISBN: 9780195748956Author: Hamisi Babusa Dontila Salee Martha Mutua Omar Babu

KES 1,100.00

Oxford Kamusi Maridhawa ya Methali ni kamusi maalum ya methali za Kiswahili iliyoundwa kwa kuzingatia muundo wa kisasa wa ufundishaji unaolenga kukuza umilisi wa lugha kwa wanafunzi. Kamusi hii imeandaliwa kwa mtindo ulio wazi na rahisi ili kumsaidia msomaji kuelewa kwa kina methali mbalimbali za Kiswahili. Kila methali imefafanuliwa kwa kueleza maana yake ya nje na ya ndani.

Mbali na kutoa ufafanuzi wa methali, kamusi hii pia inaonyesha mifano ya matumizi yake katika mazungumzo na katika maandishi mbalimbali ya kitaaluma. Kupitia maelezo hayo, mwanafunzi ataweza kujifunza namna sahihi ya kutumia methali katika utunzi wake kama vile wa insha, hadithi, hotuba na tungo nyingine za Kiswahili.

Aidha, kamusi hii imeboreshwa zaidi kwa kujumuisha visawe na vinyume vya methali zote. Hii itamsaidia msomaji kuelewa methali zinazofanana kimaana pamoja na zile zinazotofautiana kimaudhui.

Waandishi wa kamusi hii ni wasomi wenye tajiriba pana katika masuala ya elimu, utafiti, ufundishaji na tathmini. Wana uzoefu mkubwa na mpana katika ufundishaji wa Kiswahili katika viwango mbalimbali nchini Kenya.

Buy from Nuria Kenya

Buy from Text Book Centre

Description

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Oxford Kamusi Maridhawa ya Methali”

Your email address will not be published. Required fields are marked *