Description
Oxford Kiswahili Fasaha ni msururu ulioandikwa kwa njia ya kipekee na unaokidhi mahitaji yote ya Mtaala wa Kiumilisi.
Vitabu katika msururu huu vina shughuli anuwai ambazo zinalenga kumsaidia mwanafunzi kupata umilisi, kukuza maadili na vinashughulikia masuala mtambuko yanayokusudiwa katika mtaala.
Oxford Kiswahili Fasaha, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 11 kina:
- Shughuli mbalimbali zitakazomwezesha mwanafunzi kupata stadi zote nne za lugha – Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika – pamoja na matumizi ya lugha kimuktadha
- Sehemu za Kiangaza ambazo zinawapa wanafunzi fursa ya kueleza ufahamu wao kuhusu dhana husika
- Sehemu za Zingatio ambazo zinatoa maelezo ya kina kuhusu dhana husika
- Sehemu za Tudijitike ambazo kwazo mwanafunzi ana nafasi ya kutangamana na vifaa vya kidijitali katika kufanya mazoezi
- Michoro ya rangi inayochangia uelewa wa dhana zinazofunzwa
- Tathmini binafsi baada ya kila mada kuu ili kumsaidia mwanafunzi kupima uelewa wake wa dhana husika.
Kitabu cha Mwanafunzi kina Mwongozo wa Mwalimu.Oxford, mshirika wako katika ufanisi!




Reviews
There are no reviews yet.