Description
Mchezo huu ni tafsiri ya mmojawapo wa michezo ya misiba iliyo mashuhuri iliyotungwa na yule mwandishi wa Kigiriki, Sofokile, kiasi cha miaka 420 kabla ya Kristo. Unatuwekea mbele yetu hadithi nzuri mno ya mfalme ambaye, pamoja na kuwa na moyo laini, ana ndweo ya kiburi cha kuzawa nacho. Kiburi hicho ndicho kinachompeleka kwenye kifo kiovu baada ya kumuua babake na kumuoa mamake bila ya kujua.
Katika tafsiri hii iliyofanywa kutokana na nakala kadha wa kadha za Kiingereza, Samuel Mushi ameuhifadhi ule moyo na tabia ya ushairi asilia wa Kigiriki na papo hapo akashikamana na mwendo wa ushairi wa Kiswahili kwa kadri inavyowezekana. Katika utangulizi wake anakokoteza kwamba ingawa mchezo huu ulitungwa kwa mujibu wa utamaduni wa Kigiriki wa kale, wahusika wake na hisia zao ni za kiulimwengu mzima na, kwa hivyo, mchezo wenyewe unaweza kuchezwa katika mazingira ya Kiafrika.
Reviews
There are no reviews yet.