Description
Majaaliwa alipokutana na binadamu wenzake alitamani kujichimbia ardhini ajifiche. Waliicheka rangi yake ‘iliyochujuka,’ kama walivyosema wenyewe. Walimhepa na kumkimbia kama mgonjwa wa ukoma! Wakati mwingine Majaaliwa alijutia majaaliwa aliyopewa, lakini alijijasiri akakabiliana nayo kiume. Aliyakabali kama vile simba jike mwenye hasira anavyomkabili adui, na hatimaye! Hatimaye…
“Ni Rangi Tu” ni hadithi ya kusisimua iliyoandikwa kwa lugha sahihi. Lugha ambayo inateka makini ya msomaji na kumfanya kutaka mfululizo bila kukoma.
Reviews
There are no reviews yet.