Description
‘Kitumbua Kimeingia Mchanga’ ni tamthilia inayozusha mawazo kuhusu tofauti zilizoko baina ya mila na tamaduni za kale na za kisasa kuhusu suala la ndoa. Pia imeshughulikia uhuru wa vijana wa kileo kinyume na matakwa ya wazee wao. Fikirini hakubali kuchaguliwa mke na babake, Bw Mambo na nyanyake, Bi Hoja. Wazee wake wanaona jambo la kumchagulia mtoto wao mke ni jukumu lao. Vilevile, wanamtuhumu Hidaya, msichana ambaye Fikirini anataka kumuoa, kuwa ni kiruka njia, mhuni na muovu. Je, Fikirini atashinda kuwatoa shaka na kuwashawishi wazee wake wamkubalie analolipenda? Je, ndoa ya Fikirini itafanikiwa?
Reviews
There are no reviews yet.