Description
Majaaliwa alipokutana na binadamu wenzake alitamani kujichimbia ardhini ajifiche. Waliicheka rangi yake ‘iliyochujuka’, kama walivyosema wenyewe. Walimhepa na kumkimbia kama mgonjwa wa ukoma! Wakati mwingine Majaaliwa alijutia majaaliwa aliyopewa, lakini alijijasiri akakabiliana nayo kiume. Aliyakabili kama vile simba jike mwenye hasira anavyomkabili adui, na hatimaye! Hatimaye …
‘Ni Rangi Tu’ ni hadithi ya kusisismua iliyoandikwa kwa lugha sahili. Lugha ambayo inateka makini ya msomaji na kumfanya kutaka kuisoma mfululizo bila kukoma.
Ally Mtenzi, mwandishi wa hadithi hii ni naibu wa Mhariri Mkuu katika runinga ya K24, Shirika la Usambazaji habari la Media Max.
Reviews
There are no reviews yet.