Description
‘Mabandia’ ni tamthilia inayopiga kurunzi ubandia unaojificha na kujifichua kwa sura mbalimbali maishani. Maisha ni kama karata. Wahusika sita wanajitokeza katika maonyesho sita wakifululiza hadi barazani kucheza duru sita za mchezo maarufu wa Wahedi wa Sitini. Mchezo huu huchezwa hasa katika maeneo ya pwani ya Afrika Mashariki.
Kupitia vitendawili vinavyoibuka katika maonyesho mbalimbali, mwandishi anagubika hoja kadhaa za ubandia. Hoja hizi zinalenga kutafakarisha jinsi ubandia huo unavyoathiri mitazamo ya binadamu katika nyanja mbalimbali za maisha.
Ali Attas ni mwandishi mtajika wa vitabu kadhaa vikiwemo kamusi, vitabu vya lugha na vilevile vya hadithi. Kama mhariri wa vitabu vya elimu, mtangazaji, mwandishi habari na mwalimu wa lugha na fasihi mwenye uzoefu mkubwa, amebugia tajriba pana na za kipekee katika ukumbi wa kukikuza Kiswahili.
Reviews
There are no reviews yet.