Description
Musa na King Kong wanabaki bila mahali pa kulala baada ya ‘maonesho’ yao ya fataki kuteketeza kimakosa mabweni katika shule yao _ Mukibi’s Educational Institute for the Sons of African Gentlemen. Walioathiriwa na mkasa huo wanalazimika kupiga kambi kwenye mahema ukingoni mwa mto.
Katika harakati za kuchimba shimo la kutia mhimili wa hema, King Kong anachimbua mfuko wenye vito vya thamani. Pamoja na wenzake, wanashindwa kujiwekea siri ya ugunduzi huo mkuu, na muda si mrefu, wanajipata katika matatizo makubwa.
Reviews
There are no reviews yet.