Description
Kitaru na Juma ni vijana wawili ambao wanasoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanaotoka katika familia mbili za kikabaila ambazo zenye historia zilizofanana na zilizotofautiana. Ukabaila wa familia ya Juma ni ‘ubwanyenye’, na ukabaila wa familia ya Kitaru ni ‘unaizi’. Katika mchezo huu ukabaila wa aina ya familia ya Juma umeanza kung’olewa, lakini ukabaila wa aina ya familia ya Kitaru ndiyo kwanza unatiliwa mbolea na uzalendo. Daina ya Kitaru na Juma kuna mapenzi na chuki, shaka na wasiwasi, tuhuma na dhambi, huku wakitafuta uhusiano wa maana katika wakati na hali waliyonayo.
Reviews
There are no reviews yet.