Description
Kila mtu hufanya juhudi ili apate kufaulu maishani. Katika hali hii, ahadi nyingi hutolewa, miadi ikapangwa na mikakati kuwekwa ili kufanikisha maazimio. Utashi wa Dola na hadithi nyingine ni mkusanyo wa hadithi fupi zinazoakisi maisha ya wanadamu: hisia zao, mitazamo yao, ndoto zao, matumaini yao. Ubora wa hadithi katika mkusanyo huu haumo tu katika uanuwai wa fani bali pia kwenye mseto wa ufundi wa wachangiaji ambao wana asili na mitazamo tofauti. Aidha, hadithi hizi zimeteuliwa kwa upekee wa maudhui yanayoangaziwa, kama vile tamaa, nafasi ya mtoto wa kiume, ufisadi, dhuluma na unyanyasaji, ubinafsi, mapenzi, ndoa, usaliti miongoni mwa mengine mengi.
Hadithi hizi zimeandikwa na waandishi, mahiri na chipukizi, kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki. Mchango wao katika diwani hii ni wa kipekee na bila shaka utakupa kila sababu ya kuthamini uanuwai wa tamaduni zetu mbalimbali, zinazofanikisha umoja wetu.
Reviews
There are no reviews yet.