Description
Chifu Abdullah anaingia katika kazi ngumu kuliko zote alizowahi kuzifanya katika maisha yake, kazi ya kuisaka kanda iliyopotea katika kasri yake. Kanda yenyewe inatembea kutoka mkono mmoja hadi mwingine, huku pande mbili zinazoisaka zikitumia nguvu, pesa na akili kuitafuta.
Msako wa kanda unakutanisha watu wenye tajriba pana katika mambo ya uhalifu. Wapo wanaojeruhiwa, wapo wanaoumizwa, wapo wanaokufa kwa sababu ya kanda, hali inayoitia jeshi la polisi katika kibarua kigumu cha kuwasaka wahalifu hao.
Je, polisi watafaulu kuwapata wahalifu hao. Je, kanda yenyewe itapatikana? Hivi, ndani ya kanda kuna nini?
Reviews
There are no reviews yet.